Kocha wa Man Utd Sir Alex ametetea mshambualiji wake
tegemezi Robin Van Persie kuwa hajaishiwa kiwango. Sir Alex akiongea kupitia
United Magazine alisema “Robin bado hatujaweza kumtumia vizuri lakini sio
kwamba amekwisha kiwango, ni mazingira yetu sisi kama United ndiyo yamemfanya
kasi yake ipungue ila atarudi muda sio mrefu”. Sir Alex alieleza hayo kwa kile
kinachosemwa kuwa Robin Van Persie anasumbuliwa na msongo wa mawazo kwavile hajafunga
goli tokea February 10 baada ya mechi na Evarton. Van Persie huu ndiyo msimu
wake wa kwanza na Man utd akitokea Arsenal kwa dau la paundi milioni 24, hadi sasa ameshacheza mechi 31 na kufunga magoli 23.
No comments:
Post a Comment