Monday, April 8, 2013

Williamson kocha wa Uganda afukuzwa kazi


Shirikisho la mpira wa miguu nchini Uganda (FUFA) limemfukuza kazi kocha mkuu wa timu ya taifa Bobby Williamson. Williamson alifukuzwa kazi leo asubuhi (8/4/13) baada ya shirikisho hilo kufanya kikao cha dharura kilichokuwa kikiongozwa na Lawrence Mulindwa. Mulindwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari hakusema wazi sababu ya kumfukuza kazi kocha huyo zaidi ya kusema mkataba wake umekwisha kulingana na sheria za kazi za Uganda. Williamson alianza kazi ya kuifunidhsha Uganda mwaka 2008 na aliweza kushinda vikombe vinne vya kombe la Afrika mashariki na kati “challenge cup” . Licha ya kutoeleza sababu kubwa za kufukuzwa kazi, mashabiki wengi wa soka nchini Uganda wamesema kufungwa na Liberia goli 2 kwa bila katika michuano ya kufuzu kombe la dunia ndiyo sababu kubwa ya kocha huyo kufukuzwa, kwani hadi sasa Uganda inashikilia nafasi ya mwisho kwenye kundi 'J' ikiwa na pointi 2, kundi linaloongozwa na Senegal kwa kuwa na pointi 5, wakati Liberia wakiwa na nafasi ya pili na pointi 4, Angola nafasi ya tatu na pointi 3.  

No comments:

Post a Comment