Klabu ya Yanga baada ya kutoka
droo ya goli 1-1 dhidi ya timu ya Mgambo katika mechi iliyofanyika katikati ya
wiki hii wamesema refa aliyechezesha mchezo huo hakuchezesha vizuri ndiyo maana
wamepata matokeo mabaya na kusababisha kuumia kwa wachezaji wao. “Refa wa
mchezo hakuwa ‘fair’ kabisa, alikuwa anawapendelea sana Mgambo, rafu nyingi
alikuwa anaziachia kitu ambacho kimesababisha Yanga kupata majeruhi saba” hayo
ni maneno yake Baraka Kiziguto msemaji wa klabu ya Yanga alipohojiwa akiwa Mabatini
Kijitonyama kwenye mazoezi ya Yanga leo jioni. Wakati huo huo daktari wa Yanga
amesema wachezaji sita kati ya hao walioumia siku ya mechi na Mgambo
wanaendelea vizuri lakini Juma Abdul bado hali yake sio nzuri hivyo atahitaji
muda zaidi ili aweza kupata nafuu. Yanga wapo kwenye maandalizi dhidi ya Ruvu
JKT mchezo utakaofanyika jumapili ya April 21 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment