Azam FC leo inashuka uwanjani jijini Rabat Morocco kwenye michuano ya CAF Confederations Cup huku ikiwa na rekodi yakucheza michezo mitano bila kupoteza hata mmoja. Azam FC leo inahitajika kushinda au kutoka sare ya magoli ili iweze kusonga mbele katika michuano hiyo ikiwa ni muwakilishi pekee wa Tanzania aliyebakia kwenye michuano ya kimataifa. Uwezo wa kusonga mbele upo na wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wamekuwa wakifanya mazoezi ya nguvu tokea jumanne ya wiki nchini Morocco, ikumbukwe Morocco walifungwa goli tatu na Taifa stars katika michuano ya kufuzu kombe la dunia hivyo Azam FC nao wakijituma na kucheza kama walivyozoeleka basi matokoe ya mwisho yatawafanya wasonge mbele. Azam FC katika nafasi ya ushambuliaji itawategemea sana John Bocco ambaye ndiye mfungaji bora wa ligi msimu uliopita na Kipre ambaye ni mfungaji bora wa ligi msimu huu. Naye kocha msaidizi wa Azam Kali Ongara amesema kiufundi wamejiandaa vizuri, kwani wameweza kuangalia tena michezo ya wapinzani wao kwenye video na waliweza pia kuwaangalia wakicheza katika mechi ya ligi wiki hii, kupitia mafunzo hayo wamejipanga vizuri kuwakabili na kuleta ushindi kwa Azam FC. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa leo Mei 4 majira ya saa moja usiku kwa masaa ya Afrika mashariki.
No comments:
Post a Comment