Mgombea aliyeenguliwa jina lake katika uchaguzi mkuu wa TFF mwaka huu bwana Michael Wambura amesema anaishukuru FIFA kwa maamuzi iliyoyafanya na ameomba kamati ya maadili ya TFF iundwe upya na Tenga asiwepo wala asihusishwe katika kamati ya maadili ya TFF kwasababu katika mchakato uliopita aliwafanyia fitina kwa kuweka mbele maslahi yake binafsi. Wambura amesema Tenga aliingilia utendaji wa kamati za uchaguzi na rufaa za TFF jambo ambalo lilipelekea majina yao kuenguliwa na kusababisha mgogoro kwenye uchaguzi wa TFF. Wambura ameyasema hayo baada ya FIFA kuagiza mchakato wa uchaguzi wa TFF uanze upya baada ya uchuguzi wa shirikisho hilo kugundua baadhi ya dosari ambazo imeagiza zirekebishwe kabla ya uchaguzi kufanyika.
No comments:
Post a Comment