Serena kushoto na Maria wakiwa wameshikilia zawadi zao baada ya mchezo. |
Serena Williams amefanikiwa kutwaa kombe la Mutua Madrid open baada ya kumpiga kwa seti mbili mfululizo 6-1, 6-4 mpinzani wake mkubwa Maria Sharapova. Maria Sharapova anayeshika nafasi ya pili duniani angeshinda mechi ya leo angeweza kushika namba moja lakini bahati haikuwa kwake na kumfanya Serena aendelee kushikilia nafasi ya kwanza. Mchezo wa leo ulitarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutoka na uwezo wa Serena na Maria lakini Maria alionekana kuzidiwa kwa seti zote mbili. Huu umekuwa ni ushindi wa 50 kwa Serena katika maisha yake ya tenesi na amepata zawadi ya dola za kimarekani mil 5. Maria Sharapova itambidi ajipange vizuri kwenye michuano ijayo ya French open ili aweze kumpiku Serena kwenye nafasi ya kwanza.
Highlights ya fainali Serena vs Maria
|
No comments:
Post a Comment