Kiungo mkongwe wa Manchester United Paul Scholes ametangaza
rasmi kustaafu soka kwa mara ya pili. Scholes alishatangaza kustaafu soka mwaka
2011 lakini Sir Alex alimuita tena kujiunga na kikosi cha United mwaka 2012
mwezi wa kwanza ili kuimarisha sehemu ya kiungo ya klabu hiyo. Scholes aliweza
kucheza mechi kadhaa licha yakuwa kiwango chake hakikuwa kama
ilivyotarajiwa kutokana na umri wake. Scholes mwenye miaka 38 amethibitisha
kustaafu kwa mara ya pili na kusema hatarudi tena dimbani ili awaachie vijana
nafasi, licha yakuwa ataendelea kushughulika na kazi mbalimbali za klabu hiyo
akiwa kama balozi wa Man utd. Scholes anatarajiwa kucheza katika mechi ya
kumuaga Sir Alex Ferguson dhidi ya Swansea itakayofanyika katika uwanja wa Old
Trafford, mechi ambayo itakuwa ya mwisho kwake pia ndani ya dimba la Man utd. Scholes alijiunga na United mwaka 1993 hadi leo ameshacheza mechi 491
na kufunga magoli 107 kwa Man utd na kwenye timu ya taifa ameshacheza mechi 66
na kufunga magoli 14.
No comments:
Post a Comment