Jezi mpya zilizotolewa na klabu iliyopanda daraja kuingia ligi kuu nchini Uingereza Cardiff city zimepondwa kwa kuwa na kiwango cha chini. Jezi hizo zimeonekana kuwa na rangi tofauti kati ya bukta na shati licha ya kuwa zote ni nyekundu. Utofauti wa rangi hizi umezifanya jezi hizo kupoteza mvuto kiasi cha kuifanya kampuni ya Puma iliyotengeneza jezi hizo kushushwa hadhi yake. Vilevile mashabiki wa klabu hiyo kwa nyakati tofauti wamesema uongozi wa klabu yao umewashangaza sana kwani haijawahi kutokea klabu kuwa na jezi zenye kiwango cha chini kama hicho. Kufuatia jambo hili uongozi wa Cardiff umesema utalitolea ufafanuzi jambo hilo ndani wiki hii ili kuondoa mzozo uliopo kuhusiana na jezi hizo. Zifuatazo ni picha zinazoonesha jezi hizo ambazo zina rangi tofauti juu na chini.
No comments:
Post a Comment