Mechi ya kirafiki kati ya Brazil na England ipo kwenye hatihati ya kutofanyika baada ya mahakama ya jiji la Rio de Janeiro nchini Brazil kuahirisha mechi hiyo. Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kitengo cha mashataka cha jiji hilo kupeleka maombi mahakamani kuomba mechi hiyo isichezwe kwasababu usalama wa kiwanja cha Maracana kwenye ni mdogo. Maracana ndiyo kiwanja ambacho kinatarajiwa kutumika kwenye mchezo huo bado kipo kwenye matengenezo nje na ndani ya kiwanja jambo ambalo limesemekana ni hatari kwa watumiaji. Uongozi wa kiwanja hicho pamoja na shirikisho la mpira nchini Brazil wamepeleka pingamizi lao mahakamani kwa kile wanachosema kiwanja ni salama na kipo tayari kutumika kwenye mchezo huo wa jumapili. FA na FIFA wao wamesema pamoja na kuwa uwanja bado upo kwenye matengenezo wanaamini kila kitu kitakwenda sawa na mechi itafanyika licha ya kuwa na vipingamizi kwani uwanja huo ulishatumika mwezi uliopita kwenye mechi ya ufunguzi na hakuna taarifa zozote mbaya za kiusalama hadi sasa. Mechi hii kati ya Brazil na England ni ya kirafiki iliyopangwa kufanyika jumapili hii ni moja kati ya mechi zilizopo kwenye kalenda ya FIFA lakini vilevile inatumika kuiandaa Brazil na kombe la dunia mwakani |
Friday, May 31, 2013
Mechi ya Brazil na England matatani kufanyika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment