Aliyekuwa kiungo wa Chelsea na wa timu ya taifa ya Ureno Deco amepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu ili kusisimua misuli kwa kutumia dawa haramu iitwayo diuretic furosemide. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, alipatikana na hatia hiyo kufuati kucheza zaidi ya uwezo wake na kupelekea ushindi wa klabu ya Fluminense dhidi ya Boavista tarehe 30 mwezi uliopita. Dawa hiyo ya diuretic iliyopigwa marufuku ina uwezo wa kuficha dawa zingine za kusisimua misuli. Hata hivyo mawakili wa mchezaji huyo wamesema si kweli kwamba Deco alitumia dawa hizo ila tatizo hilo lilisababishwa na vitamini zilizoharibika mwilini mwake sababu ambazo zimesemekana ni za uongo. Nayo klabu yake ya Fluminense imesema haiwezi kusema lolote kuhusiana na jambo hilo hadi hapo uchunguzi zaidi utakapo kamilika. Mchezaji huyo wa Ureno mzaliwa wa Brazil, alishawahi kuichezea Barcelona na baadaye kujiunga na Chelsea kwa muda wa miaka miwili kuanzia mwaka 2008 hadi 2010. Deco alimeshawahi kushinda kombe la UEFA champions mara mbili akiwa na Barcelona na Porto 2006 & 2004 pia alikuwa ni moja kati ya viungo bora daniani lakini kiwango chake kilishuka na hatimaye kwenda nchini Brazil kumalizia muda wake wa kucheza soka.
No comments:
Post a Comment