Saturday, May 4, 2013

Gerrerd aiponda Everton na mashabiki wake

Kepteni wa Liverpool Steven Gerrard amewaponda wachezaji na mashabiki wa Everton baada ya kusikia wanajisifia kuwa watamaliza ligi juu ya Liverpool. Gerrard alisema “kama Everton watamaliza ligi juu yetu ni juu yao wenyewe na mashabiki wao, kwasababu kwao kumaliza ligi juu yetu ni jambo kubwa lakini sisi tulishazoea, kwani tumeshamaliza juu yao mara 51, lakini wao hii itakuwa mara ya pili. Sisi tumeanza ligi lengo letu ni kushinda ubingwa wa ligi sio kushindana na Everton. Mwaka huu tumeshashindwa kuchukua ubingwa wa ligi na kwasasa tunajipanga na msimu ujao licha ya kuwa mechi yetu dhidi ya Everton tutacheza ili tushinde kama tutafungwa itakuwa ni matokeo ya mchezo kama tulivyopoteza michezo mingine”. Gerrard aliyasema hayo kwa uchungu kwani matarajio yake ni kushinda kombe la ligi ambalo hajawahi kushinda tokea aanze kucheza mpira. Gerrard mwenye umri wa miaka 32 ameshashinda mataji na vikombe vyote nchini Uingereza ikiwa ni pamoja na kuwa mchezaji bora wa Uingereza lakini hadi sasa hana taji wala hajawahi kushika kombe la ligi kuu nchini Uingereza hivyo akili yake yote kabla hajamaliza muda wake wa kucheza soka anataka ashinde kombe la ligi. 

No comments:

Post a Comment