Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Lukas Podolski
hataondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu kwani yeye ndiye chaguo lake kuziba
pengo la Van Persie. Wenger alisema “Podolski ni mfungaji mzuri, bado anajifunza mfumo wetu wa kucheza kwani hajacheza mechi nyingi na Arsenal ndiyo maana bado hajaonesha uwezo wake, ila nampa nafasi msimu ujao acheza kama mfungaji naamini ataweza kuimudu nafasi
aliyokuwa akicheza Van Persie”. Wenger aliongeza kwa kusema kuwa “wachezaji
wengi wa Arsenal wanang’ang’ania kucheza kama wafungaji wa mwisho (namba
tisa na kumi) licha ya kuwa wao ni wazuri kwenye kiungo na winga ndiyo maana wakati
mwingine inabidi tumchezeshe Podolski kama winga na wao tuwapatie nafasi ya
kucheza kama wafungaji hali hii inamfanya Podolski achelewe kujifunza kwasababu tunamhamisha mara kwa mara
lakini msimu ujao itabidi tumchezeshe kwenye nafasi yake ili aweze kuonesha
uwezo wake. Lukas Podolski alijiunga na Arsenal msimu huu akitokea Cologne ya
Ujerumani kwa paundi milioni 11 hadi sasa ameshafunga magoli 14 akiwa na
Arsenal.
No comments:
Post a Comment