Klabu ya Liverpool ya England imedhibitisha kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ajax Cape town nchini Afrika ya kusini mwezi huu wa tano tarehe 21. Akiongea kuhusu matayarisho hayo mkuu wa mkoa wa jiji la Cape Town bwana Grant Pascoe amethibitisha hilo na kusema mji wa wake upo tayari kuwapokea Liverpool pamoja na mashabiki wote wa Liverpool kutoka bara la Afrika. Tiketi za mechi hiyo zitakuwa zikiuzwa katika supermarket zote za Shoprite nchini Afrika ya kusini kuanzia Mei 9 kwa randi 150 hadi 350. Haya wapenzi wote wa Liverpool wakati ndiyo huu kwenda kuwaona live kina Gerrard, Suarez na Martin Skrtel |
Tuesday, May 7, 2013
Liverpool kucheza mechi ya kirafiki Afrika ya Kusini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment