Imesemekana kuwa kocha wa Real
Madrid Jose Mourinho ataondoka na Xavi Alonso Real Madrid na kuhamia naye
Chelsea mwishoni mwa msimu huu. Hayo yamethibitishwa na gazeti la independence
baada ya kumhoji Alonso na kukiri kuhusiana na jambo hilo. Xavi Alonso amesema hawezi kusaini
mkataba wake mpya na Madrid mwaka huu kwani ana mipango mingine licha ya kuwa hakuweka wazi kwamba atakwenda Chelsea, ila alitaja Mourinho kuwa ni rafiki yake sana na atakuwa naye daima. Vilevile Jose mwenyewe alishawahi kutajwa Alonso kuwa ni kipenzi chake, na alisema popote atakapo kwenda angependa kuwa naye. Ila watu wengi wamehoji
kama Alonso atajiunga na Chelsea na wakati huo huo Lampard akaendelea kuwepo
nani atakuwa kwenye kikosi cha kwanza, lakini tathimini zinaonesha kuwa Lampard
atangojea hadi hatua za mwisho wa usajili ili kuona mazingira ya Chelsea kabla
hajaamua kusaini mkataba mpya au kuhamia Galaxy Marekani. Jose Mourinho ambaye ameshatamka wazi kuhamia Chelsea msimu ujao atahitajika kulipa paundi milioni 12 kwa Real Madrid kama gharama za kuvunja mkataba, pesa ambazo imethibitika zitalipwa na Chelsea.
No comments:
Post a Comment