Kocha mpya wa Man utd David Moyes anatarajiwa kuwachukua
wachezaji wawili wa Everton kwenda nao United. Wachezaji hao ni beki wa kushoto
Leighton Banes na kiungo Maroune Fellaini ambao wote ni wachezaji tegemezi kwa everton.
Moyes anatarajiwa kutumia kiasi cha paundi mil 39 kuwasajili wachezaji hao. Uamuzi
huu umeleta maswali mengi kwa baadhi ya mashabiki wa soka wakihoji uwepo wa
Baines utamzibia nafasi Evra au Evra atamzibia Baines kwani wachezaji hawa
wote wanacheza namba moja na Evra bado hajaonesha mapungufu yoyote ya
kutafutiwa mbadala wake. Vilevile kwa upande wa Fellaini anayecheza nafasi ya
kiungo atakuwa kwenye upinzani mkali kupata namba dhidi ya Carrick, Ceverley,
Kagawa na Giggs. Lakini mwisho wa siku kocha ndiye muamuzi wa mwisho atapanga
nani wa kukaa benchi.
No comments:
Post a Comment