Mchezaji namba mbili duniani kwa ubora wa tenesi Andy Murray amethibitishiwa na daktari wake kuwa hataweza kushiriki kwenye michuano ya French open nchini Ufaransa ambayo imeshaanza hatua za awali tokea jana Mei 21. Taarifa za daktari zimemuumiza sana Murray ambaye kwa kipindi cha mwaka sasa amekuwa akifanya vizuri hadi kufika nafasi ya pili, nia na malengo ya Murray ilikuwa ni kushiriki michuano hii ili aweze kuongeza pointi za kumuwezesha kufika namba moja, lakini kukosekana kwake kutasababisha Federrer na Nadal waliochini yake waweze kumsogelea na hata kumpita kitu ambacho kitamfanya atumie nguvu za ziada ili kuwapita tena. Murray amefikia hatua ya kutoshiriki michuano hii baada ya kuumia mguu na mgongo kwenye michuano ya Madrid mwezi huu. Hii itakuwa ni mara ya kwaza kwa Murray kukosa michuano ya French open tokea aanze kucheza tenesi ya kimataifa.
|
Murray akiwa na daktari wake leo asubuhi |
|
Murray siku alipoumia Madrid open |
No comments:
Post a Comment