Wachezaji wanne wikiendi hii walikuwa mashujaa kwenye vilabu vyao baada ya kufunga magoli ya muhimu. Wakwanza juu kushoto ni Frank Lampard, wikiendi hii aliweza kuifungia Chelsea magoli mawili yaliyoiwezesha kutoka na ushindi muhimu wa goli 2-1 dhidi ya Aston Villa. Sturridge juu kulia, jumapili ya jana aliweza kufunga magoli matatu (hat trick), magoli yaliyoipa ushindi Liverpool wa goli 3-1 dhidi ya Fulham. Rio Ferdinand wa chini kushoto, jumapili ya jana aliweza kufunga goli la ushindi katika mechi muhimu ya kumuaga Sir Alex Ferguson na kulia chini ni Callum Mcmanaman winga wa Wigan ndiye alikuwa chachu ya ushindi kwa Wigan katika mechi ya fainali FA kati ya Man city na Wigan, mechi iliyoisha kwa Wigan kushinda goli 1-0. |
Sunday, May 12, 2013
Lampard,Strurridge,Rio & Callum mashujaa wa wiki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment