Kocha wa Manchester United amesema hana mipango ya kustaafu hata baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa kocha huyo atafanyiwa upasuaji baadaye mwaka huu. Ferguson, 71, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kiuno baada ya kukamilika kwa msimu huu. Ferguson anasema upasuaji huo hautaharibu mipango yake ya hapo baadaye na ana matumaini makubwa kuwa ataendelea na majukumu yake kama kawaida ndani ya uongozi wa United akiwa kama balozi na mkurugenzi. Mbali ya upasuaji huo wa kiuno vilevile Sir Alex atatibiwa pua yake ambayo inavuja damu mara kwa mara ugonjwa uliokuwa nao kwa muda mrefu. Maradhi haya ndiyo moja ya sababu zilizomfanya Sir Alex kutangaza kuachia ngazi hata hivyo madaktari wamethibitisha kuwa Sir Alex atatibiwa na kupona mapema. Get well soon babu!!!
No comments:
Post a Comment