Niyonzima akiwa Pemba |
Kiungo wa Kinyarwanda Haruna Niyonzima leo amewadhibitishia wana Yanga kuwa yeye yupo kambini na hajenda popote. Akiongea kutoka uwanja wa Migombani mjini Chakechake Pemba, Niyonzima amesema "mimi nipo na timu na sijaenda sehemu yoyote, nimetoka na timu Dar es salaam na tumekuja wote Pemba kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba, ninachoweza kusema wale wanaosema kuwa sipo kambini wataeleza vizuri siku ya tarehe 18 uwanjani". Niyonzima amesema maneno hayo baada ya uvumi ulioenea mtaani kuwa ametoroka kambi na amekwenda nje ya nchi. Akizungumizia swala hilo pia, afisa habari wa Yanga bwana Baraka Kizuguto amesema habari hizo ni sio za kweli bali ni popaganda za Simba, na amewahakikishia wana Yanga kuwa wachezaji wote wapo kambini na mwalimu anaendelea kuwafunza vijana kikamilifu ili kumuua mnyama jumamosi.
No comments:
Post a Comment