Monday, June 17, 2013

Je wachezaji wote wa Man utd watakubali?

Kampuni ya magari ya nchini Marekani Chevrolet imeiomba klabu ya Man utd kuongea na wachezaji wake ili wakubali kutumia magari ya kampuni hiyo kila siku wanapokwenda kufanya mazoezi. Kampuni ya Chevrolet  imesema ipo tayari kuwapa wachezaji hao magari mapya bure ila kwa mashariti ya kuyatumia kila siku wanapokwenda na kurudi mazoezini msimu mzima wa 2013/14. Jambo hili linaonekana ni gumu kwasababu kila mchezaji wa Man utd ana gari lake analolipenda hivyo itakuwa ni kazi ngumu kuwabembeleza hadi wakubali, lakini mazungumzo bado yanaendelea kati ya Man utd na wachezaji wake. Moja ya magari mapya ambayo kampuni ya Chevrolet imejitolea kuwapa wachezaji wa Man utd ni Camaro na Corvette
Gari hili ni Chevrolet Camaro mpya ya mwaka 2013, wachezaji wengi watalichagua gari hili kwani ndiyo aina mpya ya kisasa kwa kampuni ya Chevrolet.  
Mbali ya kuanza kuwashawishi wachezaji wa Man utd kuanza kutumia magari ya kampuni hiyo, kwasasa wapo baadhi ya wachezaji wa Man utd wanaotumia Chevrolet akiwemo........ 
Flash: Left back Patrice Evra in his black Chevrolet
Evra 
Different: Defender Jonny Evans in a white version of the Chevrolet
Evans 

No comments:

Post a Comment