Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imefungwa na Morocco magoli 2-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia uliochezwa nchini Morocco. Goli la Tanzania lilifungwa na Kiemba dakika ya 62. Katika mchezo huo Morris wa Tanzania alipewa kadi nyekundu katika dakika ya 39 kipindi cha kwanza jambo lililopelekea Tanzania kuzidiwa kimchezo kwenye kipindi cha pili. Mbali ya kufungwa, timu ya Taifa ilifanikiwa kucheza mpira mzuri tofauti na tulivyozoea kucheza kwa kubutua na kufungwa magoli mengi. Matokeo ya mchezo huu yanaifanya Tanzania kuendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 6, Ivory coast bado ipo kileleni kwa pointi 10, Morocco ya tatu kwa kuwa na point 6, Gambia inashikilia mkia pointi 1. Mechi ijao Taifa stars itacheza na Ivory coast kwenye uwanja wa Taifa tarehe 16 Juni. TaifaStars XI iliongozwa na Kaseja, Kapombe, Nyoni, Yondan, Morris, Domayo, Sureboy, Kiemba, Ngassa, Samatta na Ulimwengu. |
No comments:
Post a Comment