Katika
takwimu za ubora wa viwango vya soka duniani zilizotolewa na FIFA leo zimeonesha
Tanzania imeweza kupanda kwa nafasi saba kutoka nafasi ya 116 hadi nafasi ya
109 duniani na ndani ya Afrika Tanzania imekwea hadi nafasi ya 32 wakati
Kenya ikiwa nafasi ya 123 duniani na nafasi ya 35 Afrika na Uganda ipo nafasi
ya 93 duniani na nafasi 24 Afrika. Tokea kocha Kim Poulsen aanze kuifundisha Taifa
Stars, Tanzania imekuwa ikipanda kwenye renki za FIFA kila mwezi kwani
alipoanza kufundisha, Taifa Stars ilikuwa nafasi ya 145 duniani na sasa ipo
nafasi ya 109 akiwa ameipandisha kwa nafasi 36 ndani ya kipindi cha mwaka
mmoja. Historia inaonesha Tanzania iliwahi kufikia nafasi ya 65 duniani mwaka
1995 ikiwa ndiyo nafasi ya juu iliyowahi kufikia na ilishawahi kushuka hadi
nafasi ya 175 mwaka 2005 ikiwa ndiyo nafasi ya chini kuwahi kufikiwa na
Tanzania. Hivyo Kim Poulsen ana kazi ya kuivunja rekodi iliyowekwa mwaka 1995
na ataweza kufikia hatua hiyo kama Tanzania itafanikiwa kusonga mbele kwenye
michuano ya kufuzu kombe la dunia inayoendelea sasa. Kuangalia orodha nzima ya FIFA bofya hapa
No comments:
Post a Comment