Saturday, June 15, 2013

Wachezaji wa kuwatizama kwenye Confederation

Edinson Cavani of Uruguay
Edinson Cavani (Uruguay) ni mshambuliaji wa Napoli kwa kifupi wanamuita mtambo wa kutafuta na kufunga magoli, atakuwa kwenye kikosi cha Uruguay akisaidiana na Luis Suarez, usikose kumkodolea macho kuangalia uwezo wake kwani ni moja ya wachezaji anayetarajia kuwika kwenye michuano hii na ikumbukwe kuwa ni mfungaji bora wa ligi ya Italia msimu huu 2012/13. Hadi sasa Cavani anahitajika na klabu za Chelsea, Man city na Madrid, lakini kocha wake mpye Benitez amekuwa mgumu kumuachia Cavani kwasababu anajua ndiye chachu ya ushindi kwa Napoli. 
Shinji Kagawa of Japan and Manchester United
Shinji Kagawa (Japan) ni mchezaji ambaye kiwango chake kinajulikana licha ya kuwa hajaweza kuonesha uwezo wake akiwa na Man utd msimu uliopita kutokana na ugeni ndani ya klabu, lakini kiwango chake akiwa na timu ya taifa kinatambulika, ndiye amekuwa chachu kwa timu ya taifa ya Japan kuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwakani nchini Brazil. Leo usikose kumtazama Kagawa katikati ya dimba akikimbizana na viungo wa Brazil kwenye mechi ya ufunguzi.
Neymar
Neymar da Silva Santos Júnior (Brazil) ametajwa sana kwenye vyombo vya habari kuwa ndiye mchezaji atakayewika kuliko wote msimu ujao wa ligi barani Ulaya kutokana na kiwango chake, lakini washabiki wengi wa soka duniani walikuwa hawajapata wasaa mzuri wa kuona kiwango chake kutokana na ushabiki mdogo wa ligi ya Brazil aliyokuwa akichezea, lakini michuano hii ya Confederation itatoa nafasi kwa mashabiki wa soka duniani kumuona uwezo wake akiwa na timu yake ya taifa Brazil. 
Juan Mata
Juan Mata (Hispania) amepata tuzo ya kuwa mchezaji bora ndani ya klabu yake ya Chelsea kwa msimu ulikwisha na pia alikuwa moja kati ya wachezaji waliokuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora kwenye ligi ya Uingereza. Mafanikio haya ndiyo yamemfanya Mata apate jina kubwa mbele ya Xavi, Iniesta na Fabregas jambo ambalo linamfanya aonekane kuwa ndiye nyota wa timu ya Hispania. Sifa hizi zinamfanya Mata pia kufikiriwa kuwa moja kati ya wachezaji watakao ng'aa kwenye michuano hii ya Confederation cup akiwa na kikosi cha Hispania ambacho kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hili.  
Mario Baliotelli
Mario Balotelli (Italia) a.k.a 'Why always me' uwezo pia unajulikana. Alijiunga na Ac Milan akitokea Man city na amefanikiwa kufunga magoli 12 kwenye msimu wake wa kwanza na vilevile atakumbukwa kama shujaa wa Italia kwenye michuano ya Euro iliyofanyika mwaka jana kwenye nchini za Poland na Ukraine kwa kuiwezesha Italia kufika fainali za michuano hiyo. Balotelli anasifika kwa kufunga magoli kiulaini, licha ya kuwa magoli yake mengi yanakuwa ni muhimu kwa timu hasa kwenye timu ya taifa, hivyo tunatarajia kuona kitu kutoka kwa Mario kwenye michuano hii.

No comments:

Post a Comment