Wachezaji wa Nigeria wameshindwa kusafiri kuelekea Brazil kufuatia mzozo kuhusu malipo ya ziada ya wachezaji. Timu hiyo ya Super Eagles, inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza siku ya Jumatatu, lakini wamesalia nchini Namibia baada ya mechi yao ya kufuzu kwa kombe la Dunia. Wachezaji wa Nigeria, hawajafurahishwa na uamuzi wa kuwapa dola elfu mbili kila mmoja, baada ya timu hiyo kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Namibia mjini Windhoek. Wachezaji hao wamesisitiza kuwa shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria ni lazima iongeze fedha hizo maradufu kabla ya wao kusafiri. Ripoti zinasema kuwa wachezaji hao wamesema kuwa hawawezi kusafiri kuelekea Brazil hadi mzozo huo utakapotatuliwa. Kuna wasi wasi kuwa mabingwa hao wa Afrika huenda wakakosa kushiriki katika fainali za kombe la shirikisho, itakayo anza tarehe kumi na tano hadi tarehe thelathini mwezi huu.
No comments:
Post a Comment