Marion Bartoli akiwa ameshikilia ngao yake baada ya kushinda mechi ya fainali ya Wimbledon dhidi ya Sabine Lisicki kwa seti mbili mfululizo za 6-1, 6-4. Hii ni mara ya kwanza kwa Bartoli kushinda kombe hili, na leo itakuwa ni siku ya kihistoria katika maisha yake. Mbali ya ushindi huu wa Bartoli, Wimbledon ya mwaka huu ilishuhudia wakongwe wengi ambao walitarajiwa kutwaa kombe hili kutolewa katika roundi za awali akiwemo Serena, Maria Sharapova, Na Li, na Carlone W. Kutolewa kwa wakongwe hawa kumeifanya michuano hii ipoteze raha yake kwa vile walioingia fainali (Bartoli na Lisicki) ni wachezaji waliokuwa na mashabiki wachache, licha ya kucheza mchezo safi wa kuvutia tokea raundi ya tatu hadi fainali. Fainali ya wanaume itafanyika kesho jumapili ambapo Djokovic atapambana na mwenyeji Murray. |
No comments:
Post a Comment