![]() |
Kiungo wa Brazil Paulinho jana alitoa machozi wakati akiwaaga mashabiki na wachezaji wenzake wa timu ya Corinthians nchini Brazil. Paulinho ambaye amesajiliwa na Tottenham kwa paundi mil 17, alingojea michuano ya Confederation iishe ili aweze kupata muda wa kuongea na wanafamilia wa klabu ya Corinthians ambao alikuwa nao kwa kipindi kirefu. Paulinho alisema ' napenda kuwajulisha kuwa msimu ujao nitakuwa Tottenham, lakini sitaweza kuwasahau nyinyi (washabiki, wachezaji na viongozi wa Corinthians) kwasababu ndiyo mmenifanya nifikie hapa nilipo, naondoka lakini nitarudi tena nyakati zijazo nikiwa bado fiti, asanteni sana'. Paulinho ndiye mchezaji mkubwa wa kwanza kusajiliwa na Tottenham mwaka huu, na katika kuimarisha timu, klabu ya Tottenham vilevile inafanya mazungumzo na Barcelona ili kumsajili David Villa. |
Monday, July 1, 2013
Paulinho atangaza rasmi kuhamia Tottenham
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment