Picha hii inamuonesha mchezaji wa mpya wa Real Madrid Gareth Bale akitoka kufanyiwa vipimo leo asubuhi baada ya kuumia jana usiku kabla ya mechi kati ya Real Madrid na Getafe. Ripoti ya madaktari imesema Bale hajaumia sana, hivyo itamchukua wiki moja kupona. Bale alipata majeraha katika paja wakati akifanya mazoezi kabla ya mechi jana usiku na kusababisha kocha amuondoe kwenye orodha ya wachezaji waliocheza. Katika mchezo huo Real Madrid ilishinda magoli 4 - 1, magoli ya Madrid yalifungwa na Ronaldo (2), Isco na Di Maria. |
Monday, September 23, 2013
Gareth Bale majeruhi, kukaa nje wiki moja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment