Leo Messi (kushoto) akitoka nje ya uwanja akiwa ameinama chini baada ya kuumia kwenye mchezo wa wikiendi kati ya Almeria na Barcelona. Messi alipata majeraha kwenye kipindi cha pili dk 73 na kuomba atoke nje. Majeraha hayo ni ya pili kumpata Messi kwenye paja la mguu wake wa kulia na ripoti imesema ataweza kukaa benchi kwa kipindi kisichopungua wiki mbili. Kutokana na kuumia Messi atakosa mechi moja ya Uefa dhidi ya Celtic wiki, mechi tatu za ligi na mechi moja na timu yake ya taifa Argentina. Kukosekana kwa Messi uwanjani kwa kipindi cha wiki mbili, kutampa nafasi Neymar kutawala kwenye safu ya ushambuliaji. Kipindi hiki kitakuwa ni mtihani mkubwa kwa Neymar kwani washabiki wanataka kuona kama Neymar ataweza kuziba pengo la Messi uwanjani. Neymar ataanza kuonesha kipaji chake jumanne ya wiki hii wakati Barcelona watakapokuwa ugenini kucheza na Celtic, timu ambayo ilishawahi kuwafunga Barcelona kwenye misimu iliyopita. |
Monday, September 30, 2013
Messi majeruhi wiki mbili...Neymar kutamba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment