Robert Pires (kulia) mchezaji wa zamani wa Arsenal akiongea na Ozil kwenye mazoezi ya Arsenal jana jioni. Pires ni moja ya wachezaji waliounda kikosi cha Arsenal cha mwaka 2003-04, kikosi ambacho hadi leo ni historia kwa klabu ya Arsenal na duniani kwa ujumla, kwani walicheza mechi zote za ligi bila kufungwa hata mechi moja. Pires ameungana na wachezaji wa sasa wa Arsenal ili kuwapa mawazo na kuwashauri akiwa kama mchezaji mkongwe. |
Walcott pia alikuwepo kwenye mazoezi pamoja na kocha Wenger. Walcott ni majeruhi ataweza kukaa nje kwa wiki mbili hadi tano. |
No comments:
Post a Comment