Luis Suarez akishangilia goli la pili kwa kuonesha picha ya mke wake na mtoto wake. Huu ni ujio wa Suarez baada ya kukaa nje tokea ligi ianze akitumikia kifungo cha mechi kumi nje ya uwanja. Katika mechi ya leo Suarez ameweza kufunga magoli mawili ikiwa ni ishara tosha ya kuonesha kuwa yeye bado ni moto wa kuotea mbali. |
Suarezzzzzzzzzzzzzz. Picha hii inaonesha Suarez akifunga goli la pili dhidi ya Sunderland. Mbali ya magoli mawili ya Suarez, pia Sturridge alifunga goli na kuifanya Liverpool kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Sunderland. Hadi sasa Sturridge ana magoli 5 na ndiye mfungaji wa Liverpool, lakini ujio wa Suarez unaweza kumfanya Sturridge akapunguza kasi. |
No comments:
Post a Comment