CHRIS SMALLING ni beki wa kati alichezeshwa kama beki wa kulia. Alishindwa kupanda na kushuka, alikosa kasi na maarifa ya kucheza pembeni. MAROUANE FELLAINI, ni mchezaji mgeni, alichezeshwa kama kiungo mshambuliaji, lakini aina yake ya uchezaji haina uwezo wa kujenga mashambulizi kama ambavyo Paul Scholes alivyokuwa akicheza, alishindwa kabisa kumtengenezea mipira Rooney na Welbeck. ANTONIO VALENCIA, alishindwa kucheza na Smalling. Kwa kawaida beki wa kulia na winga wa kulia lazima wacheze kwa ushirikiano, lakini Valencia na Smalling walishindwa kushirikiana kwenye ulinzi na ushambuliaji. ASHLEY YOUNG, alishindwa kucheza vyema kwenye winga ya kushoto. Young alipoteza mipira mingi na hakuwepo kabisa kwenye mchezo, hakuwa tishio kabisa. Ni bora angecheza Luis Nani kwenye nafasi ya Young, kidogo angeonesha uhai kwenye winga ya kushoto. Haya ndiyo maoni ya MARTIN KEOWN mchambuzi wa soka kwenye mtandao wa Sportsmail kuhusiana na udhaifu wa Man utd kwenye mchezo uliopita dhidi ya Man city ambapo Man utd walifungwa magoli 4-1.
|
Tuesday, September 24, 2013
Wachezaji wanne chanzo United kufungwa na City
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment