Kiungo wa klabu ya Rayo Vallecano, Raúl Baena, amesema si yeye aliyekuwa na lengo la kutosalimiana na Lionel Messi. 'Mimi sikuwa na mawazo ya kutosalimiana na Messi, nilimpa mkono lakini yeye aligoma kunisalimia. Nashangaa vyombo vya habari vinanisema mimi, picha zinajionesha wazi kuwa nilitoa mkono ila yeye hakutoa wake'. Hayo ni maelezo ya Baena, kiungo wa Rayo, alipokuwa akielezea kitendo kilichotokea wikiendi iliyopita ambapo yeye na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hawakusalimiana kabla ya mchezo baina ya Barca na Rayo, hadi sasa haijajulikana kisa cha kutosalimiana wachezaji hawa. Angalia video hapo chini kuona tukio lenyewe..... |
Tuesday, September 24, 2013
'Sio mimi, ni Messi ndiye aligoma kutoa mkono'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment