Young Africans inaendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola-Mabibo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumamosi dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Mchezo wa jumamosi ni muhimu kwa timu ya Young Africans kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake na kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya timu inayoongoza kwa tofauti ya pointi 5. |
Thursday, September 26, 2013
Yanga yaendelea na mazoezi kujiandaa na Ruvu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment