Thursday, December 12, 2013

Kilimanjaro nafasi ya nne, Kenya bingwa CECAFA

Kilimanjaro stars yashika nafasi ya nne baada ya kufungwa na Zambia kwa penati 6-5. Mchezo kati ya timu hizi ulikwisha kwa droo ya goli 1-1, magoli yalifungwa na Kampamba (Zm) na Samatta (Tz) kwa timu zote kabla ya mikwaju ya penati. Wachezaji wa Kilimanjaro Stars waliopata penalti ni Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi'. Waliokosa ni Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani.

Jubilant Kenya players at Cecafa Cup
Timu ya Kenya ndiyo mabingwa wa michuano hii mwaka huu baada ya kuifunga timu ya Sudan kwa magoli 2-0. Ushindi huu kwa Kenya umefuta historia mbaya iliyokuwa nayo timu ya Kenya baada ya kukaa miaka kumi bila kombe hili. Magoli yote mawili ya Kenya dhidi ya Sudan yalifungwa na Wanga. 

No comments:

Post a Comment