Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika Young Africans Sports Club leo usiku wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa El Max Haras El Hodod jijini Alexandria tayari kwa mchezo marudiano kati ya mabingwa watetezi Al Ahly.
Kikosi cha Young Africans kilichowasili mchana wa leo jijni Alexandria kikitokea jijini Cairo kimefanya mazoezi katika uwanja huo utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kesho, huku morali ya wachezaji kuelekea mchezo huo ikiwa ni ya hali ya juu sana.
Wachezaji 20 waliopo Alexandria wamefanya mazoezi chini ya makocha Hans Van der Pluijm, Charles Mkwasa pamoja na kocha wa makipa Juma Pondamali anayewanoa magolikipa na kuhakikisha wanaendelea kuwa fit kwa ajili ya mchezo huo.
Kesho kikosi cha mdachi Hans kitaingia uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Nadir Haroub "Cannavaro" katika mchezo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam na kuhakikisha kinapata ushindi na kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Kuelekea mchezo wa kesho ambao utaonyesha na televison zaidi ya 8 za nchini Misri, maandalizi yote yameshakamlika na katika kikao cha maandalizi ya mechi kamisaa ameendelea kusisitiza kuwa mchezo hautakua na mashabiki wa aina yoyote.
Mechi itachezwa kuanzia majira ya saa 1kamili kwa saa za Misri sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, na kesho wapenzi, wadau na wanachama wa Young Africans watapatiwa link ya kuweza kutazama mchezo huo moja kwa moja kwa kutumia internet. Endelea kufuatilia habari za blog hii kupata link za mchezo huu
No comments:
Post a Comment