Friday, April 18, 2014

Sita kuwania tuzo ya mchezaji bora England April 27

Steven Gerrard - Liverpool
Eden Hazard - Chelsea 
Adam Lallana - Southampton
Daniel Sturridge - Liverpool
Luis Suarez - Liverpool
Yaya Toure - Manchester City


Deadly duo: Suarez and Sturridge have been in stunning form this season for Liverpool
Washambuliaji hawa wawili wa Liverpool, Suarez na Sturridge wameonesha umahiri mkubwa wa kufunga magoli kwenye ligi ya England ikiwa hadi sasa wanaoongoza kwa kufanya magoli (Suarez 29 na Sturridge 20) na kuwafanya watengeneze historia ya pekee ndani na nje ya England. Mchezaji mmoja kati yao atachaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi licha ya kuwa mshindi kati yao lazima atoe shukrani kwa mwenzake kutokana na ushirikiano baina yao uliyofanya wafanikiwe. 

Title hopeful: Gerrard is determined to lead Liverpool to their first title in 24 years this season
Ni ukweli kwamba Steven Gerrard atakuwa na nafasi kubwa kushinda tuzo hii kama klabu yake Liverpool itaendelea kuongoza msimamo wa ligi na hata kushinda kombe la ligi. Hadi sasa mchezaji huyu ameonesha kiwango kizuri ndani ya uwanja na zaidi kuwapa hamasa wachezaji wenzake ili kucheza kwa kujituma. Ushindi wa Gerrard kwenye tuzo hii hautakuja kutokana na uchezaji wake ndani ya uwanja, bali pia uzalendo aliyouonesha kwa klabu yake akiwa kama mchezaji mahiri aliyeweza kudumu kwenye klabu ambayo ilikuwa msindikizaji kwenye ligi.

Yes to Yaya? Toure has been an imposing presence at the heart of Man City's midfield this term
Mbali ya kuwa majeruhi na kuwa nje ya uwanja hadi msimu ujao, kiungo wa Man city Yaya Toure tayari ameonesha kiwango kizuri msimu huu na kumfanya awe mchezaji tegemezi kwa klabu yake. Yaya hadi sasa ameshafunga magoli 18 akiwa kiungo pekee anayeshindana na washambuliaji kwenye kinyang'anyiro cha ufungaji magoli. Matokeo mabaya ya Man city katikati ya wiki pamoja na majeraha aliyonayo ndiyo sababu pekee zinazoweza kumpotezea ushindi wa tuzo hii lakini Yaya ataendelea kuwa kiungo bora wa msimu huu wa ligi.  

Hazard warning: The Chelsea maestro is in the running for the prestige award this season
Eden Hazard pia yupo kwenye nafasi kubwa ya kushinda tuzo hii akiwa ndiye mchezaji mwenye mvuto zaidi ndani ya klabu ya Chelsea. Hazard ameonekana kung'aa zaidi msimu huu akichukua nafasi ya Mata ambaye alikuwa mchezaji bora wa Chelsea msimu uliyopita. Uwepo wa Mata msimu uliyopita ulifunika kiwango cha Hazard tofauti na msimu huu ambapo Hazard ameweza kupata nafasi ya kutosha kuonesha kiwango chake. 

No comments:

Post a Comment