Baada ya klabu ya Sunderland kumfukuza kazi kocha wake Paolo Di Canio, majina ya makocha ambao watachukua nafasi yake yameanza kutajwa. Franco Zola na Paul Ince ndiyo makocha ambao wamesemekana kupewa nafasi ya juu kuchukua nafasi ya Di Canio. Kwasasa Ince ni meneja wa Blackpool na Zola ni wa klabu ya Watford. Taarifa zinasema, uongozi wa klabu ya Sunderland ulifanya kikao jana na muda wowote ndani ya wiki hii kocha mpya wa klabu hii atatangazwa. Di Canio amefukuzwa kazi wiki hii baada ya Sunderland kufanya vibaya kwenye ligi, kwani hadi sasa timu ya Sunderland inashikilia mkia kwenye ligi ikiwa na pointi moja. |
Monday, September 23, 2013
Zola na Ince watajwa kumrithi Di Canio
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment