Monday, April 8, 2013

ABC mabingwa kikapu Taifa

Mwaipungu (ABC) akinyanyua kikombe 
Juma Kisoki na Erick Kahangwa wakiwa kwenye kiwango  cha juu waliiwezesha timu yao ya ABC kutwaa ubingwa wa kombe la taifa kikapu baada ya kuisambaratisha timu ya Vijana City Bulls kwa vikapu 93-81 katika mchezo uliofanyika kwenye kiwanja cha mkwakwani jijini Tanga. Kisoki alifunga vikapu 24 wakati Kahangwa alifunga vikapu 22 na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano (MVP). ABC mara ya mwisho walishinda kikombe hiki mwaka 2008. Kwa upande wa wanawake Don Bosco Lionnes waliibuka mabingwa baada ya kuwabwaga mabingwa watetezi wa kombe hilo Jeshi Stars kwa vikapu 46-36 siku ya Jumamosi. Mshindi wa kwanza na wa pili kwa pande zote za kiume na kike wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Zone Five Championship yatakayofanyika  mwezi wa nane huko Bujumbura Burundi. Mashindano ya mwaka huu yalishirikisha jinsia zote za kiume na kike katika mgawanyo wa makundi matatu kama ifuatavyo, kundi A: Savio, Vijana, Chui, Bandari na Tanga Kings, kundi B: ABC, JKT, Tanga United, Mipango na Pazi, wakati kundi C la wanawake ilijumuisha Jeshi stars, Vijana queens, Don bosco lionnes, JKT Stars na Tanga Queens.

No comments:

Post a Comment