Monday, April 8, 2013

Mbwana Samata amezidi kung'ara club bingwa Afrika

TP Mazembe imefanikiwa kuingia raundi ya pili katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuipa kipigo cha mbwa mwizi klabu ya MOCHUDI CENTRE CHIEFS ya Botswana kwa magoli 6-0 mjini Lubumbashi. Mshambuaji tegemezi wa Tanzania Mbwana Samata kama kawaida yake pia alitupia goli la nne na kufikisha magoli mawili kwenye michuano hiyo. Mbali ya kufunga goli, Samata ndiye alikuwa chachu ya magoli mengine kupatikana. Mazembe wamepita kwa jumla ya magoli 7-0  baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa goli 1-0, goli lililofungwa na Mbwana Samata. Kwa ushindi huu TP Mazembe watakutana na mabingwa wa Afrika Kusini Orlando Pirates April 20 mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment