Friday, April 12, 2013

TRA yaitaka TFF kulipa deni la mil 573

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imendeelea kuibana TFF ili iweze kulipa deni lake la shilingi milioni 573 ambalo ni jumla ya kodi iliyokuwa inatakiwa kulipa kutokana na mapato inayopata kwenye viingilio vya mechi mbalimbali. TRA wameitaka TFF kulipa deni hilo kidogo kidogo kuanzia sasa na kama TFF watashindwa kutekeleza TRA italichukulia hatua za kisheria shirikisho hilo. TRA imeitaka TFF kuanza kulipa fedha hizo kuanzia jumatatu ijayo. Mapema mwaka huu TRA kupitia wataalamu wake wa kodi, walifanya ukaguzi kwenye shirikisho hilo na kuweza kubaini kiasi hicho cha fedha ambacho kinatakiwa kulipwa. TRA imesema mojawapo ya hatua itakazo chukua iwapo TFF watashindwa kutekeleza agizo lao ni kupiga mnada baada ya mali za shirikisho hilo ikiwemo majengo yake

No comments:

Post a Comment