Saturday, August 3, 2013

Rooney kurudi dimbani leo baada ya majeraha

Back: Rooney will make his return against Real Betis in a closed doors friendly
Mshambuliaji wa Man utd Wayne Rooney anatarajiwa kurudi dimbani leo kwenye mechi ya kirafiki kati ya Man utd na Real Betis. Rooney alikuwa majeruhi kwa kipindi cha wiki mbili, anatarajia kurudi pamoja na Javier Hernandez, Nemanja Vidic, Antonio Valencia na Nani ambao wote kwa pamoja hawakuwepo kwenye mechi za kirafiki barani Asia. Rooney alipatwa na majeraha akiwa nchini Thailand, na ikambidi arudi nyumbani kwa matibabu zaidi, jambo lilimfanya awembali na wenzake kwa muda usiopungua wiki mbili. Jambo hili lilisababisha kuongezeka kwa joto la uhamisho wa mchezaji huyu kwenda Chelsea, kwani umbali kati yake na kocha Moyes ulitoa mwanya mkubwa kwa Chelsea kuweza kuongea naye. Mbali ya nafasi waliyoipata Chelsea ya kuongea na Rooney kwa kipindi cha wiki mbili, lakini kocha wa United ameendelea kusisimama kwenye msimamo wake kuwa Rooney hauzwi na anatarajia kuongea naye tena wiki ijayo kabla ya mechi dhidi ya AIK jijini Stockholm. 

No comments:

Post a Comment