Thursday, April 4, 2013

Watano majeruhi Yanga


Wachezaji watano wa club ya Yanga watakosekana uwanjani kwa muda wa wiki moja hadi wiki mbili wakiwa majeruhi. Wachezaji hao wametajwa kuwa ni Jerry Tegete, Stephano Mwasika, Nizar Khalfan, Omega Seme na Said Mohamed. Mwasika na Nizar wanasumbuliwa na misuli baada ya kuumia kwenye mechi ya Polisi, Omega na Mohamed wanamatatizo ya paja na Tegete anasumbuliwa na goti. Wachezaji hao wote wameshaanza matibabu na wanaendelea vizuri. 

No comments:

Post a Comment