Thursday, April 4, 2013

Xavi ametimiza ahadi kwa kijana mwenye kansa


Kiungo wa Barcelona Xavi alitimiza ahadi aliyopewa na Miquel ambaye ni kijana wa miaka 10 anayeugua kansa. Xavi alikutana na kijana huyo hospitali moja nchini Hispania na kijana huyo alimwomba Xavi vitu viwili, cha kwanza aliomba kushiriki kwenye mazoezi ya Barcelona siku atakapo pata nafuu na jambo la pili alimwomba Xavi ashike kichwa chake akifunga goli lolote kwa Barcelona. Siku ya jumanne Xavi alitimiza ahadi hiyo kwa kijana Miquel baada ya kufunga goli dhidi ya PSG na kushika kichwa chake huku akishangilia kwa furaha. Xavi mwenyewe amesema anaamini Miquel atakuwa amefarijika na anamwombea nafuu ya haraka. Xavi ni mfano mzuri kwa wanamichezo wa bongo, ni jambo jema kuwafariji wagonjwa na watu wenye mahitaji sio lazima kuwapa pesa. 
Xavi aliposhika kichwa kutimiza ahadi baada ya kufunga goli dhidi ya PSG

No comments:

Post a Comment