Saturday, May 18, 2013

Hatuna mpango wa kumsajili Rooney - Wenger

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumsajili Wayne Rooney. Katika mahojiano yake na waandishi wa habari wiki hii juu ya mchezo kati ya Arsenal na Newcastle, mmoja kati ya waandishi wa habari alimuuliza Wenger kama kweli Arsenal inahitaji kumsajili Rooney, Wenger alijibu “ kwasasa hatuna mipango ya kumsaliji mchezaji yoyote, mipango yetu yote ni kushinda mechi ya jumapili dhidi ya Newcastle, vilevile, Man utd hawawezi kumuuza Rooney ni mchezaji mzuri na wao wanamuhitaji, hatutaki kuweka mazingira mabaya kati yetu na United kwasababu wao wameshasema hawamuuzi, sasa hiyo ni sababu tosha kuwa Arsenal haina mipango naye”. Wenger aliulizwa swali hili kufuatia tetesi zilizoenea kuwa Arsenal wapo kwenye mipango wa kumsajili Rooney, tetesi ambazo zimehamia kwa Chelsea baada ya Wenger kutamka wazi kuwa Arsenal haina mpango huo.  

No comments:

Post a Comment