Saturday, May 18, 2013

Updates za mechi ya Simba na Yanga

Ripoti inasema hadi sasa tiketi zimeshakwisha uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, na kama picha zinavyoonesha wapenzi wa soka wakiwa wamekaa pasipo kujua cha kufanya. Tiketi hizi zilianza kuuzwa jana na jana hiyo hiyo tiketi za bei ya chini zilikuwa zimeshakwisha. Hali inaonesha kundi la watu walionunua tiketi hizi watajitokeza mida ya jioni ili waziuze kwa bei ya juu, kitu ambacho sio cha kiungwana lakini vilevile imesemekana kuna kundi lingine la watu wameshaanza kuuza tiketi feki hivyo watu wanaombwa kuwa makini. 



No comments:

Post a Comment