Tuesday, May 21, 2013

Liverpool mbioni kumnasa Kolo Toure

Tetesi zinasema klabu ya Liverpool ipo mbioni kumsajili beki wa Man city Kolo Toure ili kuziba pengo la Jamie Carragher aliyestaafu msimu huu. Liverpool imefikia uamuzi huo ili kuweza kukamilisha uhamisho wa Toure mapema kabla ya kujaza mkataba wake ujao, kwani mkataba wa Toure wa sasa unatarajiwa kuisha mwezi wa saba na baada ya hapo atakuwa mchezaji huru, hivyo ataweza kuhamia Liverpool bila ya ada ya uhamisho. Kolo Toure tokea ahamie Man city amekuwa akitokea benchi kutokana na upinzani mkali kutoka kwa Kompany, Nastasic na Lescott na msimu huu ameweza kucheza mechi 15 tu za ligi kati ya mechi 36, hivyo Toure atakuwa tayari kwenda Liverpool sehemu yenye uhakika kupata namba baada ya Carragher kuondoka. 

No comments:

Post a Comment