Tuesday, May 21, 2013

Makundi ya CECAFA Kagame cup yatangazwa

CECAFA imetangaza makundi ya kombe la Kagame cup ambalo linazikutanisha klabu za Afrika mashariki na kati. Katika makundi hayo klabu za Tanzania zipo tatu, ambazo ni Yanga, Falcon na Simba. Yanga ipo kundi C, Falcon kundi B wakati Simba ipo kundi A ambalo ndiyo kundi la kifo.  Michuano hii inatarajiwa kufanyika nchini Sudan kuanzia tarehe 18 Juni hadi 2 Julai. Makundi ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo. 

KUNDI A: El-Merrekh -(Sudan), APR (Rwanda), Simba SC (Tanzania), Elman (Somalia) - EL FASHER

KUNDI B: Al-Hillal (Sudan), Tusker (Kenya), Al Nasri (Sudan Kusini), Falcon (Zanzibar),  Al Shandy (Sudan) - KADUGLI

KUNDI C: Yanga SC (Tanzania), Express (Uganda), Ports (Djibout), Vitaloo (Burundi) - EL FASHIR


No comments:

Post a Comment