Sunday, May 12, 2013

Manchester United watwaa kombe mara ya 20

Klabu ya Manchester United leo wamekabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza katika mechi yao ya 35 dhidi ya Swansea mechi iliyokwisha kwa Man utd kushinda goli 2-1. Mechi ya leo ilikuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki wa soka duniani ikiwa maalumu kumuaga Sir Alex Ferguson aliyeingoza Man utd kwa kipindi cha miaka 27. Vilevile, Paul Scholes aliyejiunga kwa mara ya pili na Man utd mwaka 2011 naye pia leo ameagwa na washabiki wa Man utd ikiwa ni mechi yake ya mwisho kucheza kwenye dimba la Old Trafford. Mechi ya leo pia imetengeneza historia kwa Robin Van Persie mchezaji aliyesajiliwa kutoka Arsenal msimu huu na leo amefanikiwa kushinda kombe la ligi kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake ya soka. Naye, Rio Ferdinand katika mechi ya leo aliweza kufunga goli la ushindi, goli ambalo amelifunga baada ya kukaa miaka mitano bila goli. Katika hotuba yake baada ya mechi, Sir Alex Ferguson amewatakia mafanikio mema wachezaji wote wa Man utd pamoja na kuwashukuru washabiki wote wa Man utd kwa kumpa “support” kipindi chote alichoitumikia klabu na kuwaahidi kuwa ataendelea kuwa nao daima. Kwaheri Sir Alex Ferguson!!!! 

Your turn: Ferguson hands the trophy over to his players before he gets covered in champagne

Let's get this party started: Sir Alex Ferguson lifts his 13th and final Premier League trophy
Sir Alex ndiye aliyenyanyua kombe la ubingwa ikiwa ni ishara ya shukrani  kwa mafanikio aliyoyafanikisha ndani ya klabu

One last time: Sir Alex Ferguson lifted his 13th Premier League trophy after watching his side beat Swansea at Old Trafford
Robin van Persie  Rooney
Robin Van Persie (kushoto) akinyanyua kombe la ligi kwa mara ya kwanza katika maisha yake
What a line-up: United players wait for the trophy presentation by lapping up the cheers

Moyes Ferguson
Kocha David Moyes na Sir Alex wakiwaaga washibiki wa timu zao baada ya mechi 
Strike out: Ferdinand's rocket wins the game for Manchester United - and big celebrations follow (below)
Rio akiachia shuti la nguvu kuandika goli la pili
Rio Ferdinand
Rio akishangilia goli la ushindi, likiwa ni goli lake la kwanza baada ya miaka mitano
Off for good: Scholes applauds the crowd as he is substituted off during his final home appearance
Paul Scholes akiwaaga mashabiki wa Man utd waliojitokeza Old Trafford 

No comments:

Post a Comment