Thursday, May 23, 2013

Sheria mpya ya UEFA, Bingwa wa Europa kushiriki moja kwa moja Uefa champions

Shirikisho la mpira wa miguu Ulaya Uefa limepitisha sheria mpya ambayo itaiwezesha timu bingwa wa Europa league kupata tiketi ya kushiriki moja kwa moja michuano ya Uefa champions. Uamuzi huo umefikiwa leo jijini London ambapo kikao cha kamati kuu ya Uefa kilifanyika. Sheria hiyo itawezesha pia nchi moja kuwa na klabu tano kwenye michuano ya Uefa champions kama bingwa wa Europa league atamaliza nafasi ya tano au chini kwenye ligi. Vilevile, Uefa imepitisha sheria ya ubaguzi wa rangi ambapo mchezaji yoyote atakayegundulika amefanya kitendo hicho atafungiwa kucheza mechi 10 na mashabiki watakao husika na kitendo hicho watasababisha uwanja kufungiwa na kufanya klabu yao icheze bila watazamaji. Sheria hizi mpya zinatarajiwa kutangazwa rasmi ijumaa ya wiki hii jijini London siku moja kabla ya fainali za Uefa champions kati ya Munich na Dormund. 

No comments:

Post a Comment