Monday, May 27, 2013

Mourinho ni baba yangu, ananijua vizuri sana, nitakuwa naye anapokwenda - Essien

Kiraka wa Chelsea Michael Essien anayecheza kwa mkopo Real Madrid anatarajiwa kurudi darajani na Jose Mourinho kutokana na mpenzi yaliyopo baina yao. Michael Essien amethibitisha hilo katika mahojiano yake na Mailsports zaidi akiweka wazi mahusiano aliyonayo na Jose “Tuna mahusiano mazuri sana na Jose, huwa namuita Baba naye ananiita kijana wangu, nina mjua vizuri na yeye ananijua vizuri na anatambua kuwa naweza kucheza namba yoyote isipokuwa golikipa, ndiyo maana anipenda, kwasababu ninaweza kuzipa pengo lolote ndani ya timu, hivyo nategemea tutakuwa wote huko aendako” hayo ni maneno ya Essien ambaye tokea ajiunge na Real Madrid ameshacheza kwenye nafasi zaidi ya mbili kuziba mapengo ya majeruhi. Mourinho anatarajiwa kujiunga na Chelsea mwisho wa msimu huu baada ya kumalizia mechi ya mwisho kati ya Real Madrid na Osasuna Juni 1. 

No comments:

Post a Comment